17th September, 2018
Wakazi wa mtaa wa ruiru wana sababu ya kutabasamu baada ya kupokea taarifa kwamba kufikia mwezi desemba mwaka huu watatumia njia ya maji taka iliyojengwa kwa kima shilingi bilioni 2.9. mtaa huo unadhaniwa kuwa na idadi ya watu 100,000 na umekuwa ukikumbwa na tatizo la maji taka tangu jadi ambapo maji taka huelekea katika mto wa ruiru ambao pia unatumika kwa maji ya matumizi mjini ruiru. Gavana wa kiambu Ferdinard Waititu amesema mradi huo wa milioni 80 utawasidia pakubwa wenyeji kwa kuimarisha hali ya afya.