.
16th September, 2018
Je, usalama katika Kanda la Afrika Mashariki limetiliwa maanani?
Siasa za Kanda linaangazia swala hili la usalama baada ya mauaji kuripotiwa katika sehemu kadha wa kadha katika kanda hili.
Viongozi katika kaunti ya Mombasa wamelalamikia ongezeko la magenge ya uhalifu mjini Mombasa na kutoa wito wa kufufuliwa kwa mpango wa nyumba kumi.
Viongozi hao kutoka kwa kamati ya amani Mombasa wakiongozwa na mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir wamelaani mauaji ya kiholela katika mji wa Mombasa na kuitaka serikali kutofanya mageuzi katika idara ya polisi kwa pupa.