15th September, 2018
Wanafunzi wa chekechea katika kaunti ya Nairobi watakuwa wanapata maziwa ya bure shuleni, hii ni baada ya gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko kuzindua mradi wa kutoa maziwa ya bure.
Mradi huo ambao ni ushirikiano wa serikali ya kaunti ya Nairobi na kampuni ya maziwa ya Brookside unatarajiwa kung'oa nanga juma lijalo.
Itakumbukwa miaka ya themanini na tisini seriklai ya rais mustaafu Daniel Arap Moi ilikuwa inatoa maziwa ya bure kwa shule za msingi kote nchini almaarufu 'maziwa ya Nyayo'.