Mwili wa mwanawe Sharon Otieno yazikwa Homa Bay

KTN News Sep 14,2018


View More on Dira ya Wiki

Mwili wa mwanawe Sharon Otieno, mwanafunzi wa shule ya upili ya Rongo aliyeuawa wiki iliyopita kwa hali ya kutatanisha, hii leo ulizikwa katika  shamba la wazazi wa Sharon Homa Bay. 

Mtoto huyo ambaye alikuwa tumboni mwa mamake wakati wawili hao walipouawa baada ya Sharon kudungwa kwa kisu alikuwa wa kwanza kuzikwa ili kutoa nafasi ya kuanza utaratibu wa kumzika mamake. 

Mazishi hayo hayakuhudhuriwa na mwanasiasa yeyote bali  familia ya Sharon na wanakijiji pekee. Sharon, ambaye inadaiwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Gavana wa Migori Okoth Obado, bado atasalia kwenye hifadhi ya maiti , kwani familia haijaanza utaratibu wa mazishi yake.