Viongozi watoa kauli kuhusu sukari bandia

KTN News Sep 12,2018


View More on KTN Leo

Katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyakazi COTU Francis Atwoli ameitaka serikali kuhakikisha kwamba sukari ya magendo inayodaiwa kuwa ya kampuni ya Mumias inaondolewa katika maduka.

Sukari hiyo ambayo inapakiwa ndani ya karatasi ambazo hazina tarehe inayoonyesha ni lini ilitengezwa, inaripotiwa kuwa madukani.

Aidha kiongozi huyo wa COTU ametaka kutekelezwa kwa asilimia tano ya nyongeza ya kima cha chini cha mishahara ya wafanyakazi ilivyodokezwa siku ya wafanyakazi( labor day) mwaka huu.