Viongozi kutoka Mlima Kenya wafanya kikao cha maji

KTN News Sep 11,2018


View More on KTN Leo

Viongozi wa eneo la mlima kenya wamekutana na waziri wa mazingira na misitu na yule wa maji kuhusiana na kukatwa kwa mabomba ya maji 660 eneo hilo. Hatua hiyo ikiibua ghadhabu za wakazi na viongozi kwenye kaunti kama meru, nyandarua, tharaka nithi, nyeri na kirinyaga. Lakini leo serikali imeafikiana kurejesha maji na kukarabati mabomba miongoni mwa hatua zingine.