8th September, 2018
Ushindi wa alama 17?0 dhidi ya Mean Machine na alama 22?5 dhidi ya Northern Suburb cubs uliisaidia kcb kutinga robo fainali ya mashindano ya dala sevens yaliyoandaliwa katika uwanja wa ask mamboleo kaunti ya kisumu hii leo.nondies pia waliingia kwenye hatua ya robo fainali baada ya kuwalaza wenyeji rfc 17?5 na mku thika alama 36?7.timu zingine ambazo zilitinga robo fainali ni viongozi wa msururu wa raga nchini Homeboyz rfc pamoja na mwamba ambao waliwashinda impalla 22?19.