Madai ya ubakaji Moi girls

KTN News Aug 31,2018


View More on Leo Mashinani

Uchunguzi kuhusiana na madai ya ubakaji wa mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya wasichana ya moi miezi mitatu iliyopita umeendelea kuzingirwa na kizungumkuti baada ya aliyekuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo rael muriithi kutetea uwezekano wa tendo hilo kutokea akisisitiza kwamba kumekuwa na usalama wa kutosha kuwadhibiti wanafunzi hao dhidi ya matukio ya aina hiyo. Hata hivyo muriithi amekwepa kudokeza iwapo anao ufahamu wowote kuhusiana na mshukiwa wa tendo hilo akisistiza kwamba suala hilo lingali linachunguzwa na vitengo husika. Aidha usimamizi wa kampuni ya usalama ya lavingtone sawa na mlinzi aliyekuwa kwenye zamu siku ya kisirani hicho wamesimama kidete kwamba usiku unaodaiwa kutokea tendo hilo hawakuona jambo lolote geni na kwamba usalama ulikuwa shwari.