Familia katika Kaunti ya Busia wapoozwa na ugonjwa usiojulikana

KTN News Aug 30,2018


View More on Leo Mashinani

Watoto watatu wa familia moja katika kijiji cha obipor eneo bunge la  teso kusini kaunti ya busia wamekumbwa na ugonjwa usiojulikana.wazazi wa watoto hao wameeleza kuwa mmoja wa mtoto wao  aliye na umri wa miaka kumi na minane na wawili pacha walio na umri wa miaka kumi na miwili walizaliwa wakiwa na afya nzuri lakini walipofika umri wa miaka mitano wakaanza kupooza katika mazingira ya kutatanisha. Wanasema watoto hao walipokea chanjo zote zinazohitajika ikiwemo chanjo ya ugonjwa wa kupooza au polio. Kwa mujibu wa mtaalamu wa maswala ya viungo katika hosipitali  ndogo ya rufaa ya alupe, jude taabu amesema kuwa ulemavu unaowakumba watoto hao unahitaji matibabu ya hali ya juu.