30th August, 2018
Msako wa wafanyikazi kutoka mataifa ya kigeni wasiokuwa na vibali vya kufanya kazi humu nchini umeimarshwa katika kaunti ya kajiado. Akizungumza kwenye mskao huo naibu kamishana wa kajiado ya kati charles wambugu amesema msako huo utaendelea na kuhakikisha kuwa wananchi hao wa kigeni wamefuata sheria kabla ya kuruhusiwa kufanya kazi humu nchini. Wambugu amesema shughuli hiyo itaendeshwa katika maeneo yote ya kajiado kwa mujibu wa agizo lililotolewa na waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matian'gi.