Ziara ya Theresa May nchini Kenya

KTN News Aug 30,2018


View More on Leo Mashinani

Waziri mkuu wa uingereza Theresa May yuko nchini kwa ziara ya siku moja katika ziara inayochukuliwa kuwa muhimu zaidi katika uhusiano wa kibiashara kati ya uingereza na kenya.  Ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka thelathini tangu waziri mkuu wa uingereza kuizuru kenya. May yuko katika ziara ya mataifa matatu ya afrika   na yuko kenya baada ya kuzuru afrika kusini. Ziara hii inakuja muda mfupi kabla ya uingereza kujiondoa rasmi katika umoja wa ulaya EU.