Viongozi pwani wakisia Kenya iwatume wanajeshi Uganda dhidi ya dikteta Museveni

KTN News Aug 26,2018


View More on KTN Leo

Naibu Gavana wa mombasa, wabunge wawili na shirika la haki africa sasa wanataka nchi ya uganda kukombolewa kwakile wanachotaja kama uongozi wa kiimla baada ya kukamatwa na kuzuiliwa kwa mwanamuziki mashuhuri ambaye pia ni mbunge Robert Kyagulanyi, maarufu kama bobi wine. viongozi hao wamesema kuwa ikiwa hatua hazitachukuliwa  huenda tatizo hilo likaenea maeneo mengine afrika. walizungumza hivi leo katika mkesha wa kuwasha mishuma  ya kumkumbuka Bobi Wine.