25th August, 2018
Wanaharakati wa shirika la kijamii katika Kaunti ya Bungoma wametishia kuelekea kortini kushtaki Bunge la Kaunti hiyo kwa ubadhirifu wa fedha .Hii ni baada ya bunge la Kaunti hiyo kushindwa kuwajibika katika kazi yao ya kuchunguza jinsi fedha zinavyotumika katika bunge hilo.
Kulingana na stakabadhi zinazodaiwa kuwa ushahidi kuonyesha jinsi ubadhirifu unavyoendelezwa kati ya karani wa bunge John Mosongo akishirikiana na waakilishi wadi katika bunge hilo, wanaharakati hao wanadai kuwa hawana imani na bunge hilo kwa mambo ya uwazi na uwajibikaji ndiposa wameamua kwenda kortini kwa niaba ya wakaazi wa Kaunti ya Bungoma.
Wamevitaka vitengo husika ikiwemo tume ya kupambana NA ufisadi EACC na ofisi ya kiongozi wa mashtaka ya umma kuingilia kati