Changamoto la kuhifadhi tembo nchini Kenya | LEO MASHINANI

KTN News Aug 23,2018


View More on Leo Mashinani

Hapo jana ulimwengu uliadhimisha siku ya kimataifa kuhusu ndovu kauli mbiu ikiwa ni kuleta ulimwengu pamoja kwa madhumuni ya kuwasaidia wanyama hawa. 
Siku hii ambayo huadhimishwa Agosti kumi na mbili imetengwa ili kutoa hamasisho kuhusu jinsi ya kuwalinda na kuwatunza ndovu kote duniani. 
Katika miaka ya hivi karibuni Taifa la kenya limekuwa likiweka mikakati ya kuongeza idadi ya ndovu katika mbuga zake. 
Kulingana na hesabu ya ndovu iliyofanywa mwaka jana katika mbuga za laikipia, meru, Samburu na  marsabit idadi ya ndovu humu nchini ilikuwa ni 15,317 ikilinganishwa na ndovu 14,411 waliokuwepo mwaka 2012.