20th August, 2018
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekanusha vikali ripoti kwamba mwanamuziki na Mwanasiasa Shupavu Robert Kyagulanyi Ssentamu almaarufu Bobi Wine yuko katika hali mbaya akiwa kizuizini. Katika taarifa kwa vyombo vya habari kwa mara ya kwanza akizungumzia swala la kukamatwa kwa mbunge huyo museveni ametaja ripoti za vyombo vya habari kwamba bobi wine alipigwa vibaya na kwa sasa yuko mahututi baada ya baada ya vurugu za kisiasa zilizotokea katika eneo la arua ambapo mlinzi wake pia aliuwawa kwa kupigwa risasi na polisi kuwa taarifa za uongo. Tunajiunga na Roland Ebole, mtafiti wa maswala ya kibinadamu nchini uganda na tanzania katika shirika la amnesty international.