Elimu chekechea: Watoto waruhusiwe kuenda shuleni wakiwa bado wachanga?Elimu chekechea: Watoto waruh

KTN News Aug 17,2018


View More on Leo Mashinani

Tangu kuzinduliwa kwa mtaala mpya wa elimu wa 2?6?3?3?3 unaofaa kuchukua nafasi ya mtaala uliodumu kwa muda wa zaidi ya miongo miwili, nafasi ya masomo ya watoto wadogo almaarufu baby class ilitakiwa kuondolewa kwa mujibu wa taasisi ya kuratibu mtaala nchini yaani  KICD. Masosmo kwa watoto wadogo yalifaa kuanzia umri wa miaka  minne katika daraja la kwanza la miaka miwili.

Hata hivyo masomo ya  chekechea bado yapo. Serikali za kaunti zikiwa na jukumu hili baada ya huduma hizi kugatuliwa. Swali je muongozo wa kuwepo kwa hizi shule za chekechea na mafunzo ya watoto ni upi? Kwa nini mafunzo mengi ya watoto wa kutwa yaitwayo Baby class bado yapo?