×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Madai ya kurahiwa Wabunge kuchukua hongo | Leo Mashinani

14th August, 2018

Mbunge wa Naivasha Jane Kihara sasa anadai kuwa kuna mbunge mmoja aliyemrai achukue hongo ili aiangushe ripoti kuhusu uagizaji wa sukari ya magendo nchini wakati ambapo mdahalo wa sukari ghushi umechukua mkondo mpya wa ulaji rushwa bungeni. Aidha kihara amepasua mbarika kuwa kuna wabunge waliohongwa ili kupiga kura visivyo ili kuiua ripoti hiyo iliyofaa kuweka bayana uwepo wa chembe za chuma aina ya makiuri kwenye sukari. Aidha kihara anasema kuwa viongozi kutoka mrengo wa nasa na pia wa jubilee walihusika katika kutoa rushwa kwa wanachama wao. Aliyazungumza haya huko naivasha saa chache tu baada ya mwakilishi wadi wa wajir fatuma gedi kukiri kuwarai wabunge wasiipitishe ripoti hiyo na wala sio kuwahonga. 

.
RELATED VIDEOS