10th August, 2018
Watu watatu wamefariki huku wengine kumi na wawili wakijeruhiwa vibaya baada ya kuhusika kwenye ajali ya barabarani iliyotokea katika barabara kuu ya Mombasa. Ajali hiyo iliyohusisha magari manne ilitokea mwendo wa saa tano usiku wa jana. Kulingana na kamanda wa kaunti ya Machakos Samuel Mukhindia majeruhi wanaendelea kupata matibabu katika hospitali ya machakos level 5.