Wafugaji wa Samburu watafuta soko la ng'ombe

KTN News Aug 07,2018


View More on Leo Mashinani

Wafugaji katika eneo la Samburu wanakadiria hasara baada ya kukosa soko la kuuza mifugo wao. Wafugaji hao wamesema  soko la mifugo limeporomoka  baada ya mawakala  kukoma kuja kununua mifugo wao. Sasa wafugaji hao wanalazimika kutembea zaidi ya kilomita mia moja kutoka maeneo ya baragoi kutafuta soko la kuuza ng'ombe wao.