27th July, 2018
Utafiti mpya umebaini kuwa wakenya wengi wenye imani ya dini ya kikatoliki wanatumia mbinu za kisasa za kupanga uzazi licha ya marufuku ya kanisa hilo. Kwa mujibu wa utafiti huo wa shirika la Catholic FO Choice, wakatoliki watatu kati ya watano hawakubaliani na msimamo wa kanisa kuhusu matumizi ya tembe na njia nyingine za kisasa za kupanga uzazi.
Kupitia waraka wa papa paul wa 6, kanisa katoliki lilipiga marufuku matumizi ya mbinu hizo za kupanga uzazi miaka 50 iliyopita na kuruhusu tu matumizi ya njia za kiasili kupanga uzazi. Tunajiunga na profesa Joseph Karanja, mhadhiri na mtaalamu wa afya ya uzazi katika hospitali kuu ya Kenyatta hapa jijini Nairobi.