20th July, 2018
Vita dhidi ya ufisadi vinaendelea kuzua tumbo joto miongozi mwa viongozi na ngome mbali mbali za siasa hivi karibuni ikiwa ni ile ya bonde la ufa. Mbunge wa Pokot South David Pkosing ameendeleza kauli za kuwa vita hivyo vinaielenga jamii yao,.Aidha Pkosing aliongeza kuwa vita hivyo vinalenga uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022 kwa lengo la kuizima kurunzi ya Naibu Rais William Ruto ya kumrithi Rais Uhuru Kenyatta