17th July, 2018
Waalimu wakuu na halmashauri ya usimamizi wa shule katika kaunti ya samburu wametakiwa kufanya uchunguzi utakaosaidia kuepusha mizozo inayosababisha migomo ya wanafunzi na uharibifu wa mali ya shule. Kamishna wa kaunti ya marsabit john korir ameonya waalimu wakuu kwamba watachukuliwa hatua endapo migomo itafanyika katika shule zao bila wao kujua.