Gavana wa Busia Sospeter Ojaamong asema madai ya ufisadi dhidi yake ni ya uongo

KTN News Jul 03,2018


View More on KTN Mbiu

Gavana wa kaunti ya Busia Sospeter Ojaamong amesema kwamba  madai  ya ufisadi dhidi yake ni ya uongo .Ojamoong anasema  kwamba  hajapokea ilani yoyote ya  kushtakiwa  kwake   kwa madai ya ufisadi katika kaunti hiyo . Mkurugenzi wa mashtaka ya umma  Noordin Hajj.  aliidhinisha kufunguliwa mashtaka dhidi ya gavana   huyo  kwa madai ya matumizi mabaya ya mamlaka. Inadaiwa kuwa Ojaamong alikiuka kanuni za utoaji zabuni  na hivyo kuisababishia kaunti ya Busia kupoteza mamilioni ya pesa.