Chama cha Jubilee kiko tisti, hakuna mkutano wowote wa dharura, asema Tuju

Michael Majanga Jul 02,2018


View More on KTN Mbiu

Katibu mkuu wa chama cha Jubilee Raphael Tuju amepinga madai kwamba kuna nyufa katika chama hicho. Aidha Tuju amepuuzilia mbali taarifa kuwa kutakuwa na mkutano wa wanasiasa wa Jubilee hapo kesho ili kusawazisha utata uliopo baina ya vingozi wanaoaminika kuwa wa mkono wa naibu Rais William Ruto na wale wanaodhaniwa kumuunga mkono na kumpendelea Rais Uhuru Kenyatta.