20th June, 2018
Mkufunzi wa timu ya taifa ya raga ya wachezaji 15 Ian Snook ametaja kikosi cha wachezaji 23 kitakachoshiriki mchuano wa Gold Cup dhidi ya Morocco siku ya jumamosi. Mechi hiyo aidha ni ya kutafuta nafasi ya kufuzu michuano ya kombe la dunia itakayoandaliwa nchini Japan mwakani.