Ushindi kwa magavana Waiguru na Nyong'o korti ikiidhinisha kuchaguliwa kwao

KTN Leo | Thursday 14 Jun 2018 9:02 pm

Mahakama kuu mjini Kerugoya imedumisha ushindi wa gavana wa kaunti ya Kirinyaga Anne Waiguru na kumwamuru mpinzani wake Martha Karua kulipa shilingi milioni tano kama gharama. Bi karua ambaye ni mwenyekiti wa chama cha Narc kenya amesema atakwenda katika mahakama ya rufaa kubatili uamuzi wa jaji Lucy Gitari. Akitoa uamuzi huo jaji gitari amesema kuwa karua alishindwa kudhihirisha kuwa uchaguzi wa waiguru ulikumbwa na udanganyifu.