Jamaa auawa na raia Kisumu kwa madai alimuua msichana

KTN Leo | Thursday 14 Jun 2018 7:53 pm

Raia waliojawa na hasira wamemvamia na kumpiga hadi kufa mwanamme mmoja mwenye umri wa makamo katika eneo la Car Wash mjini kisumu  kwa madai kuwa alihusika katika kifo cha msichana mmoja ndani ya nyumba yake. Inadaiwa mshukiwa huyo alikuwa akijaribu kutoroka baada ya kumuua msichana huyo na kupakia mwili wake ndani ya begi.