27th May, 2018
Gor Mahia wamefuzu raundi ya pili ya dimba la Ngao ya Sportpesa baada ya kuwatitiga SS Assad ya Mombasa mabao matano kwa moja kwenye mechi ya raundi ya 32 bora iliyochezwa uwanjani mbaraki.
Kiungo Lawrence Juma alifunga mabao mawili kwa mpigo huku Godfrey Walusimbi, Eliud Lokuwam na mshambuliaji Jakis Tuyisenge wakifunga bao moja kila mmoja kuwahakikishia Kogalo ushindi huo. Kogalo watapambana na mshindi wa mechi kati ya Kenpoly FC na Savannah Cement.