27th May, 2018
Wahudumu wa bodaboda katika kaunti ya Kisii wametaoa makataa ya siku tano kwa polisi kukomesha kukamatwa ovyo ovyo kwa wenzao la sivyo watandaa maandamano kila siku na kusambaratisha shughuli za usafiri . Wakizungumza na wanahabari muungano wa kaunti wa wanabodaboda ukiongozwa na Gisore Orechi wamewalaumu maafisa wa polisi katika kaunti ya Kisii ambao kwa madai kuwa wamekuwa wakichukua hongo. Orechi amedai kuwa zaidi ya wanabodaboda 100 wamekamatwa na maafisa wa polisi katika barabara ya kisii ? Kilgoris