26th May, 2018
Wadau wakuu hasa viongozi wa serikali kuu na wale wa kaunti ya Elgeyo Marakwet pamoja na halmashauri ya ustawi ya KVDA wameahidi kuweka kando na tofauti zao na kuhakikisha miradi mikuu ya umeme na maji katika mabwawa ya aror na Kimwarer yanafanikishwa bila fujo. Wakiongozwa na waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa, seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen na afisa mkuu mtendaji wa KVDA David Kimosop viongozi hao waliwataka wakazi kuridhia mradi huo ambao unalenga kutoa ajira kwa zaidi ya watu 2000. Mradi wa Kimwarer na Aror utaigharimu serikali bilioni 63 huku bilioni 6.3 itatumika kufidia wenyeji wa pande hizo. Awali palizuka mzozo kuhusiana na malengo ya mradi huo