25th May, 2018
Matayarisho ya mashindano ya ndondi ya "The Awakening Boxing Tournament" yataandaliwa siku ya Jumamosi ugani Impala, Nairobi huku shirikisho la ndondi nchini likizidi kujiandaa kuimarisha hali na viwango vya mchezo huo. Mashindano hayo yatajumuisha jumla ya vitengo 11 vikiwemo vile vya super middle weight, middle weight, light weight na cruiser weight. Miongoni mwa watakaoshiriki ni bondia Daniel Wanyonyi wa Kenya ambaye ndiye bingwa mtetezi wa kitengo cha super middle weight. Wanabondia kutoka nchi za India, Uganda na Tanzania pia watashiriki mashindano hayo. Aidha, wanabondia wa humu nchini wameshauriwa kuhakikisha kuwa wamefuata kanuni za sheria wanaposaini kandarasi kwa mashindano ya kitaifa na ya humu nchini ili kuhepukana na masaibu ya kukosa kulipwa.