25th May, 2018
Kocha mpya wa Harambee Stars Sebastien Migne amejikwaa katika mchuano wake wa ufunguzi huku Kenya ikilazwa na Swaziland bao moja kwa nunge. Bao hilo la wageni lilipachikwa kunako dakika ya 78 na Mandla Palma. Kocha amedokeza kwamba timu yake imepata mafunzo huku Waziri wa michezo Rashid Echesa akisema kwamba kosa moja haliachi mke.