25th May, 2018
Baadhi ya wakazi wa West Pokot wamemtaka naibu wa gavana katika kaunti hiyo kujitokeza kwani hawajamuona kwa miezi mingi. Wananchi hao aidha wanamlaumu gavana John Lonyangapuo kwa kuwa hajachukua hatua yoyote baada ya naibu wake Nicholas Atudonyang kutoonekana. Wanasema kutoweka kwake kunapelekea ukosefu wa huduma zinazotegemea afisi yake na kukosekana kwa maenedeleo. Wameapa kwamba watafanya maandamano hivi karibuni kushinikiza hatua kuchukuliwa dhidi ya Atudonyang ambaye pia anasimamia sekta ya afya katika kaunti ya West Pokot kama waziri. Msaidizi wa naibu gavana James Kodoso amesema kuwa gavana John Lonyangapuo anafahamu fika alipo naibu wake na kwamba majukumu yake yanatekelezwa.