23rd May, 2018
Waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuri ameagiza kufanyika kwa uchunguzi kuhusu sakata ya uuzaji wa mahindi katika mabohari ya NCPB . Kiunjuri amesema kuwa wakulima wanaodai fedha kutoka kwa serikali watachunguzwa na kulipwa hela zao. Kulingna na waziri kumekuwepo ulaghai katika bodi ya nafaka ambapo maafisa wamekuwa wakinunua mahindi kutoka kwengine na wala sio kwa wakulima nchini . Uchunguzi ungali unafanywa kuhusiana na sakata hiyo baada ya afisaa mkuu mtendaji wa NCPD kujiuzulu na mameneja watano kuachishwa kazi .