22nd May, 2018
Ujenzi wa nyuga nne za soka maeneo ya Dandora, Jacaranda, Kariakor na Kihumbini ulizinduliwa siku ya Jumanne papa hapa jijini Nairobi. Ujenzi huo wa viwanja hivyo vinne vinanuia kuangazia ukosefu wa nyuga za kutosha jijini huku pia mradi huo ukilenga kuwapa vijana kazi kupitia michezo.