27th April, 2018
Wawakilishi wadi wamemkosoa aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga kwa madai kuwa wanalemaza shugli za kaunti. Katika hotuba yake kwa magavana na maseneta katika kongomano la ugatuzi huko Kakamega, Odinga aliwashutumu wawakilishi wadi kuwa wanawaitisha magavana pesa/posho ili wapitishe miswada katika bunge za kaunti, pamoja na madai mengine.