27th April, 2018
Wizara ya kilimo na maji sasa imebuni halma shauri ya kitaifa itakayotwikwa jukumu la kusimamia uvunaji wa maji sawa na kudhibiti mafuriko yatokanayo na mvua ya masika.
Waziri wa maji Simon Chelugui ambaye amewarai wananchi kujihami kwa vifaa vya kuvuna maji hata hivyo amesistiza kwamba mgao wa maji jijini Nairobi utaendelea kushuhudiwa kutokana na upungufu wa maji kwenye bwawa la Ndakaini huku akishikilia msimamo kwamba kiwango cha chini cha mvua kwenye mlima aberdare ndicho chanzo cha upungufu wa maji ya kutosha kwenye bwawa hilo lililo na uwezo wa kushikilia maji lita bilioni sabini kwa wakati mmoja.