14th April, 2018
Serikali imetakiwa kutatua tatizo la ukosefu wa ajira ambao umesababisha ongezeko la ukosefu wa usalama na kukiukwa kwa haki za kibinadamu. Wakizungumza mjini Nakuru wakereketwa wa haki za kibinadam kutoka shirika la haki afrika wamesema kuwa licha ya visa vya ukiukaji wa haki wanasiasa hawajali kushughulikia suala hilo na badala yake wanajipigia debe kwa uchaguzi wa 2022