12th April, 2018
Wakazi wa Githima katika kaunti ndogo ya Thika mashariki walifanya maandamano na kufunga barabara eneo hilo wakilalamikia hali mbaya ya barabara. Maandamano hayo yalisababisha msongamano wa mamia ya magari aina ya lori. waandamanaji hao walilalamika kuwa licha ya wao kutozwa ada, hali ya barabara hizo imesahaulika. wanasema serikali ya kaunti inapata zaidi ya shilingi laki tatu katika ada wanazotozwa
kwenye barabara hiyo na kuitaka kuingilia kati.