10th April, 2018
Shughuli katika hospitali ya Kabazi katika eneo la Subukia kaunti ya Nakuru zimelemazwa baada ya wafanyikazi katika hospitali hiyo kuachishwa kazi ghafla.Kisa na maana mzozo baina yao na msimamizi wa hospitali.Inadaiwa kuwa msimamizi huyo Edward Omondi aliamua kuwafuta kazi vibarua na kwenda likizo bila kutoa sababu. Wakazi wa eneo hilo sasa wanataka msimamizi huyo ahamishwe.