10th April, 2018
Waziri wa elimu, Amina Mohamed amesema mpango wa kuwatuma walimu wengine katika kaunti ya Wajir unaendelea.Akizungumza alipofika mbele ya kamati ya bunge kuhusu elimu, Waziri Amina aliyekuwa ameandamana na afisa mkuu mtendaji wa tume ya TSC, Nancy Macharia, aliwaarifu wabunge kwamba walimu watakaotumwa katika kaunti ya Wajir, watahitajika kufanya kazi kwa miaka mitatu kabla ya kuhamishwa.Kwa upande wake, Nancy Macharia amesema uhaba wa walimu nchini umechangia matatizo yanayoikumba sekta ya elimu.