.
9th April, 2018
Wasiwasi umegubika kina mama katika hospitali ya rufaa ya Voi baada ya wanawake kulalamikia idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa na ugonjwa wa homa ya Nyongo ya manjano.Huu ni ugonjwa unaoathiri maini na ambayo athari zake ni macho kuwa rangi ya njano.Baadhi yao wana wasiwasi kuwa huenda kukazuka homa hatari zaidi, watoto wengi wakiendelea kutibiwa katika hospitali hiyo.Hata hivyo,msimamizi wa hospitali hiyo ya Voi amesema ugonjwa unaoshuhudiwa kwa sasa unawapata watoto wengi na huisha kwa muda wa siku tatu.