9th April, 2018
Mkenya Stacy Ndiwa amaliza wa pili na kutwaa medali ya fedha katika fainali za mbio za mita 10,000 huku mbio hizo zikitawaliwa na Waganda Stella Chesang aliyetwaa dhahabu na Mercyline Chelangat aliyeshinda medali ya shaba.Chesang alishinda kwa muda wa dakika 31 sekunde 45 nukta 30.huku Ndiwa akiweka muda wa dakika 31:46.36.