4th April, 2018
Wakazi wa Samburu kaskazini wameitaka serikali kuwekeza katika ujenzi wa mabwawa ili kuvuna maji ya mvua na kuyahifadhi tayari kwa wakati wa kiangazi. Wakazi hao wanasema iwapo serikali itawekeza anagalau kwa mabwawa mawili tu, itakuwa jambo nzuri kwa shughuli za kilimo na ufugaji. Wakati wa kiangazi kaunti ya Samburu huwa ni baadhi ya kaunti zinazoathirika pakubwa na ukosefu wa maji huku wakazi wakilazimika kutembea masafa marefu kutafuta maji.