30th March, 2018
Timu ya Mathare United iliishinda timu ya Chemelil Sugar bao moja kwa sufuri kwenye mchuano wa ligi kuu nchini uliochezwa ugani Kenyatta, Machakos. Bao hilo la pekee lilitiwa kimiani na Cliff Nyakeya dakika chache kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika. Kwa sasa Mathare iko kileleni mwa ligi kuu kwa alama 17 huku ikisuburi mechi za Gor Mahia, Ingwe na Bandari wikendi hii.