.
21st March, 2018
Furaha imetanda leo katika shule ya upili ya Chebuyusi baada ya mahakama ya Milimani kutupilia mbali uamuzi wa baraza la mitihani nchini KNEC kwa madai kuwa shule hiyo ilihusika na ulaghai wakati wa mtihani huo. Sasa baraza hilo limepewa makataa ya siku kumi na nne kufanya tena uchunguzi. Matokeo yaliyozuiliwa na baraza la mtihani nchini yalionyesha kuwa Chebuyusi ilikuwa ya kwanza katika kaunti ya Kakamega, ya pili katika uliokuwa mkoa wa Magharibi na ya kumi na sita kitaifa. Wazazi na wanafunzi waliwasilisha kesi mahakamani kupinga maamuzi ya KNEC katika kesi iliyosikizwa na jaji wa mahakama kuu George Odunga