20th March, 2018
Moses Wetangula ameng'olewa kwenye kiti chake cha kiongozi wa wachanche katika bunge la seneti. Mzozo huo umekuwa ukitokota ndani ya muungano wa NASA tangu nyufa zianze kuonekana kwenye muungano huo pale maseneta wa chama cha ODM kuhisi kwamba wao ndio wanastahili kiti hicho kulingana na idadi yao ndani ya seneti. Seneta wa Siaya James Orengo anakabidhiwa kiti hicho, baada ya kubainika kwamba spika Kenneth Lusaka amedinda kuipokea barua ya afisa mkuu wa NASA Norman Magaya, iliyopinga kung'olewa kwa Wetangula. Ndio mwanzo wa kusambaratika kwa NASA? Je, upinzani umekosa makali baada ya ODM kuamua kufanya kazi na serikali ya Jubilee? Na je, Raila Odinga ana ushawishi kiasi gani kwenye yale yaliyomfika Wetangula?