.
26th February, 2018
Mahakama kuu sasa imetoa agizo kwa idara ya uhamiaji kufanikisha kurejeshwa nchini kwa wakili anayekumbwa na utata Miguna Miguna. Kwenye uamuzi wake, Jaji Chacha Mwita ameiagiza idara hiyo pia kumruhusu Miguna kutumia paspoti yake ya Canada. Jaji Mwita amesema Miguna anahitajika kuwa nchini ili kuweza kutoa ushahidi kwenye kesi kuhusu uraia wake. Wakati huo huo, Jaji Mwita amebatilisha agizo la waziri wa usalama Fred Matiang'i kuratibisha vuguvugu la NRM kuwa kundi haramu.