23rd February, 2018
Timu za raga ya wachezaji saba kila upande zinapania kuboresha matokeo kwenye mechi zijazo. Timu ya wanaume almaarufu shujaa itasafiri siku ya jumamosi kuelekea marekani kwa mashindano ya las vegas sevens huku timu ya kina dada almaarufu the lionesess ikinuia kutumia mashindano ya hong kong sevens kama njia ya kujinoa kwa michezo ya jumuia ya madola.