×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Mahakama yabatilisha ushindi wa gavana wa Embu Martin Wambora: Mbiu ya KTN

22nd February, 2018

Mahakama imebatilisha ushindi wa Martin Wambora kama gavana wa kaunti ya Embu. Kwenye uamuzi katika mahakama kuu jaji William Musyoka ameamuru kuhesabiwa upya kwa kura zilizopigwa Agosti tarehe nane mwaka uliuopita, ambapo Lenny Kivuti alipinga matokeo ya uchaguzi huo. Wawili hao waliachana kwa tofauti  ya kura mia tisa themanini na tano, kwani Wambora alizoa kura tisini na saba elfu, mia saba sitini huku aliyekuwa seneta wa Embu Lenny Kivuti akipata kura tisini na sita elfu, mia saba sabini na tano.  Jaji musyoka kwenye uamuzi wake ameridhika na ushahoidi uliowasilishwa na upande wa ulalamishi kwamba vipo visa vya udanganyifu vilivyojitokeza wakati wa kura hizo.  Mahakama imebaini kwamba baada ya kuamriwa kuhesabiwa upya kwa kura hizo, tofauti kati ya washidani hao wawili ilipungua ikawa finyu hata zaidi, kwa kura mia mbili tisini na tisa. Jaji ametanabahi kwamba tume ya IEBC imekiri kuwa udanganyifu ulikuwepo katika kituo cha gategi huko Mbeere kusini. Hii si mara ya kwanza kwa gavana Wambora kupoteza ushindi wake. Kwenye muhula wake wa kwanza ushindi wake uliwahi kubatilishwa kwa tuhuma za udanganyifu.

.
RELATED VIDEOS